Pata taarifa kuu
DR Congo-Rwanda-Hague

Bosco Ntaganda kupandishwa kizimbani machi 26 katika mahakama ya kimataifa ya ICC

Kiongozi wa makundi ya uasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bosco Ntaganda aliyejisalimisha kwenye Ubalozi wa Marekani amefikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo, Ntaganda atapandishwa kizimbani siku ya jumanne machi 26 na kusomewa mashtaka yote yanayomkabili.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ntaganda aliondoka jijini Kigali ijumaa hii akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, maofisa wa ICC na wanadiplomasia, na muda mchache baada ya kuwasili ICC, mahakama hiyo imethibitisha ujio wake kupitia mtandao wa kijamii wa twitter.

Majaji wanatarajiwa kuthibitisha utambulisho wake na lugha ambayo atatumia wakati mashtaka yake yatakapoanza kusikilizwa.

Kiongozi wa ICC Fatou Bensouda ameeleza kuridhishwa kwake na ujio wa Ntaganda na kusema hiyo ni habari njema kwa waathirika wote wa mapigano ya nchini DRC ambao wanatarajia haki itapatikana kupitia mahakama hiyo.

Naye Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema wana matumaini haki itatendeka na hatua hiyo inapeleka ujumbe kwa washukiwa wengine wa uhalifu kuwa siku yao itafika nao watafikishwa katika mkono wa sheria.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.