Pata taarifa kuu
MAREKANI-PALESTINA-ISRAEL

Rais Obama aihakikishia Palestina kuwa Marekani inaunga mkono upatikanaji wa taifa lao

Rais wa Marekani Barrack Obama amezuru Mamlaka ya Palestina na kusema kuwa Marekani inaunga mkono uwepo wa taifa huru la Palestina. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na rais wa Mamlaka hiyo Mahmud Abbas mjini Ramalla rais Obama ameongeza kuwa mpango wa Israel wa kujenga makaazi ya walowezi katika ardhi ya Palestina haikuwa njia sahihi ya kupata amani katika eneo hilo.

Rais Abbas kwa upande wake amemwambia rais Obama kuwa Palestina haitashiriki katika mazungumzo ya amani ikiwa Israel itaendelea na mpango wake wa kujenga makaazi mapya katika ukingo wa Magharibi.

Obama amezuru Ramalla kwa saa kadha kabla na kurejea Bethlehem kutoa hotuba kwa raia wa Israel kuhusu uhusiano kati ya Israel na Palestina na mchango wa Marekani kuhakikisha kuwa amani inadumu katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, raia wa Palestina wanasema hawaoni umuhimu wa ziara ya Obama katika Mamlaka hiyo kwa kile wanachokisema kuwa tangu rais huyo wa Marekani alipoingia madarakani hajawafanyia chochcote .

Ziara ya Obama inakuwa ni ziara yake ya kwanza kwenye eneo la Mashariki ya kati tangu kuchaguliwa kwake kwa muhula wa pili kama kiongozi wa taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani.

Obama amemwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa ,Marekani haina rafiki wa dhati kama Israel na itaendelea kujenga uhusiano thabiti kati ya mataifa hayo mawili.

Kuhusu Iran rais Obama amesema kuwa nchi hiyo ina nafasi ya kujirekebisha kuhusu mpango wake wa Nyuklia kupitia njia za kidiplomasia kuepuka nguvu za kijeshi kutumiwa dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.