Pata taarifa kuu
ITALIA

Mchakato wa kumpata Papa mpya wa kanisa katoliki waanza mjini Roma

Makadinali wa Kanisa katoliki duniani wamekutana mjini Roma nchini Italia kuanza zoezi la kumchagua papa mpya wa kanisa hilo atakayeziba pengo lililoachwa na Papa Benedicto wa kumi na sita aliyejiuzulu rasmi mwishoni mwa mwezi uliopita. Asubuhi hii Makadinali 115 watashiriki katika misa ya pamoja kabla ya kuanza mchakato wa kumtafuta kiongozi mpya kuanzia jumanne hii.

dailymail.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Makadinali hao watapiga kura mara nne kila siku hadi theluthi mbili watakapo kubaliana kuhusu ni nani atakayekuwa kiongozi wao.

Wakati wote wa uchaguzi huo Makadinali hao watajifungia katika chumba maalum hadi pale makadinali 77 watakapoafikiana kuhusu Papa mpya.

Zoezi hili huenda likachukua siku kadhaa na papa atakayechaguliwa atakuwa papa wa 266 wa kanisa hilo na kuwaongoza wakatoliki takribani bilioni 1 nukta mbiili duniani kote.

Papa Mpya atachukua nafasi ya Papa Emeritus zamani akifahamika kama Benedicto wa kumi na sita aliyejiuzulu mwezi uliopita kwa sababu ya umri mkubwa wa miaka 85 na sababu za kiafya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.