Pata taarifa kuu
BULGARIA

Maandamano yaendelea nchini Bulgaria licha ya Serikali ya Waziri Mkuu Borisov kutangaza kujiuzulu

Maandamano yameendelea kuitikisa nchi ya Bulgaria kwa siku nyingine tena licha ya Waziri Mkuu Boyko Borisov kutangaza kujiuzulu kwa serikali yake baada ya kushindwa kushughulikia madai ya wananchi wa Taifa hilo. Maelfu ya waandamanaji wameonekana katika Mji Mkuu Sofia wakiendelea kupaza sauti kutaka kupunguzwa kwa bei ya umeme pamoja na kudhibititwa kwa upandaji wa gharama za maisha kwenye Taifa hilo.

Maelfu ya waandamanaji wakiwa mitaani nchini Bulgaria kupinga ongezeko la bei ya umeme nchini humo
Maelfu ya waandamanaji wakiwa mitaani nchini Bulgaria kupinga ongezeko la bei ya umeme nchini humo
Matangazo ya kibiashara

Watu wanaokadiriwa kufikia 2,000 wamefanya maandamano nje ya Ukumbi wa Bunge kitu ambacho kiliwasukuma polisi kutumia nguvu pamoja na mabomu ya machozi kuwasambaratisha wananchi hao.

Wananchi wa Bulgaria baada ya kuandamana kwa siku kumi mfululizo ndipo Waziri Mkuu Borisov alipojitokeza na kulihutibia Bunge na kutangaza kujiuzulu kwa serikali yake baada ya kuguswa na Polisi walivyowashambulia.

Waandamanaji hao wamesema wamefanikiwa kumuondoa mtu mmoja ambaye alikuwa mkorofi Waziri Mkuu Borisov lakini bado kuna Viongozi wengine waliosalia madarakani na wanapaswa kuondolewa pia.

Maandamano hayo yameanza kukumbwa na mgawanyiko baada ya wafuasi wa Waziri Mkuu Borisov kujitokeza mitaani wakishinikiza kurejea madarakani kwa Kiongozi huyo siku moja baada ya kujiuzulu kwake.

Waziri Mkuu Borisov alitangaza kujiuzulu baada ya kujiridhisha serikali yake kushindwa kushughulikia madai ya wananchi ambao wamewaweka madarakani na hivyo wameoja watoe nafasi kwa Viongozi wengine.

Bulgaria ndiyo nchi maskini zaidi katika Umoja wa Ulaya EU lakini ikiwa inatoza gharama kubwa zaidi za umeme ukilinganisha na nchi nyingine kitu ambacho kimekuwa kikiwanyonya mno wananchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.