Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Washia wasitisha maandamano kwa ajili ya kuzika miili ya waliopoteza maisha mwishoni mwa juma huko Quetta

Wananchi wa Pakistani kutoka Jamii ya Washia wametangaza kufanya mazishi ya ndugu zao waliouawa mwishoni mwa juma wapatao 89 kwenye mashambulizi ambayo yanatajwa kutekelezwa na Makundi ya Wasunni.

Maiti za Watu wa Jamii ya Washia waliouawa mwishoni mwa juma zinazotarajiwa kuzikwa hii leo
Maiti za Watu wa Jamii ya Washia waliouawa mwishoni mwa juma zinazotarajiwa kuzikwa hii leo REUTERS/Naseer Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Washia ambao walitia ngumu kufanya mazishi ua ndugu zao wakitaka serikali kuchukua hatua kudhibiti mauaji yanayoelekezwa kwao mara kwa mara wameridhia pia kusitisha maandamano yaliyodumu kwa siku tatu mfululizo.

Jamii ya Washia katika Jiji la Quetta imesema watafanya mazishi kutokana na kutekeleza sheria ya kiislam ambayo inawakataza kuendelea kukaa na maiti kwa muda mrefu lakini madai yao yapo pale pale.

Washia ambao ni wachache nchini Pakistan wamesema wameamua kufanya mazishi ya ndugu zao ili waendelea kuishinikiza serikali kuchukua hatua zinazofaa dhidi ya wale wanaotekeleza mauaji hayo.

Jamii ya Washia ililazimika kufanya maandamano makubwa katika Jiji la Quetta na maeneo ya Karachi, Lahore na Islamabad wakitaka serikali iwapatie ulinzi madhubuti ili waepukane na mauaji yanayofanywa dhidi yao.

Mazishi haya yanafanyika kipindi hiki ambacho serikali imefanya juhudi kubwa ya kuwashawishi Washia hao kufanya maziko ya ndugu yao wakati wakiendelea na msako wa kuwabaini waliotekeleza mauaji hayo.

Kundi la Lashkar-e-Jhangvi ndili lilijigamba kutekeleza mashambulizi yaliyochangia vifo vya washia 89 mwishoni mwa juma huku serikali ikishindwa kuchjukua hatua zozote dhidi yao.

Mwanasheria Mkuu wa Pakistan Iftikhar Muhammad Chaudhry ametaka hatua za haraka zichukuliwe ikiwemo ni pamoja na kuwakamata wafuasi wa Kundi la Lashkar-e-Jhangvi ambao wamehusika kwenye mauaji hayo.

Waziri Mkuu Raja Pervez Ashraf alilazimika kutuma mawaziri wake kueleka Kusini Magharibi mwa nchi hiyo kufanya mazungumzo na washia ili waweze kusitisha maandamano yao kitu ambacho kimefanikiwa.

Mashambulizi ambayo yalitekelezwa mwishoni mwa juma kutoka kwa Wasunni dhidi ya Washia licha ya kusababisha vifo hivyo 89 lakini yalishuhudia watu 170 wakijeruhiwa vibaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.