Pata taarifa kuu
TUNISIA

Waziri mkuu Tunisia atishia kujiuzulu ikiwa hataunda serikali mpya

Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali ametishia kujiuzulu ikiwa mpango wake wa kuunda serikali mpya hautafanikiwa huku akionya juu ya vurugu zinazoendelea kupata nguvu nchini humo.

Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali
Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Waziri Hamadi Jebali amesema atatekeleza azma yake ya kujiuzulu ikiwa atashindwa kuunda serikali mpya juma lijalo kama alivyoahidi.

Waziri Jebali amefikia uamuzi huo baada ya kuuawa kwa kiongozi Chokri Belaid ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa kwa serikali,tukio ambalo limeliingiza taifa hilo katika taswira mpya na kushuhudia ghasia wakati chama tawala nacho kikizidi kugawanyika baada ya waziri mkuu huyo kuwa katika mkakati wa kuunda serikali mpya ya wataalamu.

Wanachama wa chama kikuu cha kiislamu Enhada walipanga kuandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo siku ya jumamosi ikiwa ni siku moja tu kupita baada ya polisi kukabiliana na waombolezaji katika mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya jumatano.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.