Pata taarifa kuu
Tunisia

Waziri mkuu wa Tunisia atangaza nia yake ya kuunda serikali mpya ya kitaifa

Waziri mkuu wa tunisia Hamad Jebali ametangaza jana kwamba ataunda serikali mpya ya kitaifa ityo undwa na mawaziri wajuzi wasioegemea chama chochote baada ya kutokea mauaji ya kiongozi mkuu wa upinzani `Chokri Belaid hali iliozua ghasia kubwa nchini Tunisia.

waziri mkuu wa Tunisia
waziri mkuu wa Tunisia
Matangazo ya kibiashara

Waziri Jebali amesema ameaumuwa kuunda serikali ya kitaifa yenye wajumbe wasioegemea upande wowote wa kisiasa itayo kuwa na muhula maalum itayo kwenda hadi utapofanyika uchaguzi katika kipindi kifupi.

Hata hivyo waziri mkuu huyo hakufahamisha ni lini serikali iliopo itavunjwa wakati yeye mwenyewe akisalia kuwa waziri mkuu wa serikali mpya ambayo itahitaji uidhinishwaji wa baraza la bunge na hakutaja majina la mawaziri wapya.

Uamuzi huu unakuja wakati muungano wa mrengo wa kushoto na chama cha kiislam cha Ennahda wakivutana tangu miezi kadhaa kuhusu ugavi wa wizara huru.

Jebali amesema kwamba uamuzi huo wa kuunda serikali itayo undwa na wajumbe wasiokuwa na upande wowote wa kisiasa, ilikuwepo hata kabla ya kutokea kwa kifo cha kiongozi huyo mkuu wa upinzani
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.