Pata taarifa kuu
MISRI

Machafuko zaidi yaendelea kushuhudiwa nchini Misri huku Wapinzani wakikataa wito wa kukutana na Rais Morsi

Machafuko zaidi yameendelea kushuhudiwa nchini Misri kipindi hiki ambacho Viongozi wa Upinzani wakikataa mwaliko wa kufanya mazungumzo uliotolewa na Rais Mohamed Morsi na badala yake wametaka maandamano makubwa zaidi yaitishwe.

Polisi wakitumia bakora kuwasambaratisha Waandamanaji waliojitokeza kwenye Jiji la Cairo nchini Misri
Polisi wakitumia bakora kuwasambaratisha Waandamanaji waliojitokeza kwenye Jiji la Cairo nchini Misri Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Ghasia hizo zimeshuhudiwa katika Jiji la Cairo na kushuhudiwa vikitikisa eneo la Viunga vya Tahrir kitu ambacho kiliwapa kibarua Polisi wa kupambana na ghasia na kutumia mabomu ya machozi kusambaratisha waandamanaji.

Wanaharakati wamekuwa mstari wa mbele kupinga matumizi makubwa ya nguvu ambayo yanafanywa na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na waandamanaji ambao wamekuwa hawaridhishwi na mwenendo wa serikali ya Rais Mohamed Morsi.

Ghasia za jana pekee zilishuhudia mtu mmoja akipoteza maisha baada ya kupigwa risasi huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kutokana na Jeshi la Polisi kulazimika kutumia risasi za moto kuwasambaratisha waandamanaji.

Duru za kitabibu zimekiri waandamanaji wengi wamejeruhiwa na risasi pamoja na mabomu ambayo yalikuwa yanatumika kwenye mchakato wa kurejesha hali ya utulivu katika Jiji la Cairo.

Machafuko haya nchini Misri yanaingia siku ya sita hii leo kitu ambacho kinaangaliwa ni kama Taifa ambalo bado halijamaliza mapinduzi yaliyofanikishwa kuangushwa kwa Rais Hosni Mubarak.

Viongozi wa Upinzani wameendelea kusimama kidete na kutaka wananchi kuendelea na maandamano hayo kutokana na serikali iliyopo madarakani kushindwa kusikiliza matakwa yao.

Wito huo wa Wapinzani umepokelewa vizuri na wafuasi wao ambao kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wameendelea kusisitiza kuendelea na maandamano yao ili wapate kile walichokipigania miaka miwili iliyopita.

Haya yanashuhudiwa kipindi hiki ambacho Rais Morsi akiwa ametangaza hali ya hatari katika Miji mitatu ikiwemo Suez, Port Said na Ismailiya ambayo mwishoni mwa juma ilishuhudia ghasia kubwa baina ya waandamanaji na Polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.