Pata taarifa kuu
MISRI

Rais Morsi atangaza hali ya hatari kwenye Miji mitatu kwa siku 30 kukabiliana na ghasia ambazo zimezuka mwishoni mwa juma

Rais wa Misri Mohamed Morsi amelazimika kutangaza hali ya hatari katika Miji mitatu nchini humo ambayo ni Port Said, Suez na Ismailiya itakayodumu kwa siku thelathini kutokana na kuwepo kwa ghasia zilizochangia watu kadhaa kupoteza maisha na wengine mia nne sitini kujeruhiwa.

Ghasia zilizofanyika mwishoni mwa juma nchini Misri na kusababisha Rais Mohamed Morsi kutangaza hali ya hatari
Ghasia zilizofanyika mwishoni mwa juma nchini Misri na kusababisha Rais Mohamed Morsi kutangaza hali ya hatari REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Misri amelazimika kuchukua hatua hiyo ya kutangaza hali ya hatari kutokana na kukiri kuna kitisho cha usalama kinachochochewa na ghasia ambazo zimeendelea kutanda kwenye Miji hiyo kwa siku tatu mfulullizo sasa.

Tamko la Rais Morsi limeanza kutekelezwa mara moja ili kukabiliana na ghasia ambazo zimeshuhudiwa kwenye Miji hiyo mitatu kutokana wananchi wengi kuingia mitaani baada ya Mahakama kuwahukumu adhabu ya kunyongwa waliohusika na mauaji ya watu sabini na wanne kwenye Uwanja wa Mpira wa Miguu.

Maandamano makubwa yameshuhudiwa nchini Misri huku waandamanaji wakikabiliana vilivyo na askari ambao walikuwa kwenye dori kudhibiti ghasia zlizokuwa zinatekelezwa na watu hao ambao walionekana kuchukizwa na hukumu hiyo.

Rais Morsi tayari ameshawaalika Viongozi wa Vyama Vya Siasa kukutana naye baadaye hii leo kujadili kile ambacho kinaendelea kushuhudiwa katika Taifa hilo kutokana na uwepo wa maandamano kila uchao.

Watu thelathini na mmoja wamepoteza maisha kwenye ghasia hizo wakiwemo askari wawili wa kukabiliana na ghasia pamoja na kijana mdogo ambaye amepigwa risasi ya kifuani kwenye harakati za kuzima ghasia.

Vyombo vya Usalama vimeanza kujipanga vyema kukabiliana na kitisho chochote cha usalama ambacho kinaandaliwa na makundi ya vijana ambao wamekuwa mstari wa mbele kupanga maandamano yanayogeuka machafuko katika siku za hivi karibuni.

Wafuatiliaji wa Siasa wamekuwa wakieleza pasi na kificho kutokana na maandamano yanayoendelea kushuhudiwa nchini Misri ni wazi kabisa Umaarufu wa Rais Mohamed Morsi umezidi kushuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.