Pata taarifa kuu
MISRI

Ghasia Mpya zazuka nchini Misri ikiwa ni siku ya tano tangu kuanza kwake na mtu mmoja apigwa risasi

Ghasia mpya zimezuka nchini Misri ikiwa ni siku ya tano mfululizo kushuhudia ghasia ambazo zimekuja saa kadhaa baada ya Rais Mohamed Morsi atangaze hali ya hatari katika Mji mitatu kwa siku 30 na kuzuia wananchi kutembea nyakati za usiku.

Wananchi wenye ghadhabu wanaoupinga Utawala wa Rais Mohamed Morsi wakipambana na Jeshi la Polisi
Wananchi wenye ghadhabu wanaoupinga Utawala wa Rais Mohamed Morsi wakipambana na Jeshi la Polisi REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Ghasia hizi mpya zimechangia mtu mmoja kupigwa risasi ambaye hakuwa anashiriki kwenye maandamano hayo kitu ambacho kinatajwa kuongeza hasira zaidi kwa waandamanaji ambao wamejitokeza kwenye mitaa mbalimbali huyo Suez.

Wananchi wengi wanasema kile kinachoendelea kinadhihirisha ni kutokamilika kwa mapinduzi ambayo yaliong'oa Utawala wa Rais Hosni Mubarak kupitia nguvu ya umma lakini hata serikali ya rais Morsi inakabiliwa na hali ngumu.

Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kukabiliana na waandamanaji hao ambao wamekuwa wakirusha mawe pamoja na mabomu ya petroli kukabiliana na polisi ambao wamesambazwa mitaani.

Machafuko haya yanakuja baada ya Rais Morsi kutangaza hali ya hatari katika Miji mitatu nchini humo ambayo ni Port Said, Suez na Ismailiya itakayodumu kwa siku thelathini kutokana na kuwepo kwa ghasia zilizochangia watu kadhaa kupoteza maisha na wengine mia nne sitini kujeruhiwa.

Kiongozi huyo wa Misri amelazimika kuchukua hatua hiyo ya kutangaza hali ya hatari kutokana na kukiri kuna kitisho cha usalama kinachochochewa na ghasia ambazo zimeendelea kutanda kwenye Miji hiyo kwa siku tatu mfulullizo sasa.

Tamko la Rais Morsi limeanza kutekelezwa mara moja ili kukabiliana na ghasia ambazo zimeshuhudiwa kwenye Miji hiyo mitatu kutokana wananchi wengi kuingia mitaani baada ya Mahakama kuwahukumu adhabu ya kunyongwa waliohusika na mauaji ya watu sabini na wanne kwenye Uwanja wa Mpira wa Miguu.

Maandamano makubwa yameshuhudiwa nchini Misri huku waandamanaji wakikabiliana vilivyo na askari ambao walikuwa kwenye dori kudhibiti ghasia zlizokuwa zinatekelezwa na watu hao ambao walionekana kuchukizwa na hukumu hiyo.

Rais Morsi tayari ameshawaalika Viongozi wa Vyama Vya Siasa kukutana naye baadaye hii leo kujadili kile ambacho kinaendelea kushuhudiwa katika Taifa hilo kutokana na uwepo wa maandamano kila uchao.

Watu thelathini na mmoja wamepoteza maisha kwenye ghasia hizo wakiwemo askari wawili wa kukabiliana na ghasia pamoja na kijana mdogo ambaye amepigwa risasi ya kifuani kwenye harakati za kuzima ghasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.