Pata taarifa kuu
LIBYA

Uingereza, Ujerumani na Uholanzi zawataka raia wake wanaoishi mjini Benghazi nchini Libya kuondoka

Nchi za Uingereza, Ujerumani na Uholanzi zimewataka raia wake wanaoishi na kufanya kazi mashariki mwa nchi ya Libya kwenye mji wa Benghazi kuondoka kwenye mji huo na kurejea nyumbani kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama. 

Ubalozi wa Marekani mjini Benghazi ukiteketea kwa moto baada ya kushambuliwa mwaka jana
Ubalozi wa Marekani mjini Benghazi ukiteketea kwa moto baada ya kushambuliwa mwaka jana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema kuwa kuna taarifa ya kwamba raia wakigeni hasa wa nchi za Magharibi wamekuwa wakiwindwa na makundi ya kiislamu ambayo yanapinga harakati za mataifa hayo katika nchi za ukanda wa kiarabu na mashariki ya kati.

Wizara hiyo imewataka wananchi wake wote wanaoishi mjini Benghazi kuondoka kwenye mji huo mara moja na kurejea nyumbani ili kuepuka utekaji nyara ambao umekuwa ukifanywa kwa siri na baadhi ya makundi ya kiislamu nchini humo.

Kwa upande wake Serikali ya Uholanzi imewataka wananchi wake wawe makini kwenye mji wa Benghazi na miji mingine ya mashariki mwa nchi hiyo kutokana na kuwepo kwa taarifa za kuzorota kwa usalama kwenye maeneo hayo.

Serikali ya Berlin kwa upande wake yenyewe imesema kuwa wamepata taarifa kuhusu kuwepo kwa makundi ya kiislamu kwenye mji wa Benghazi ambayo yanalenga kuanzisha uasi dhidi ya raia wa kigeni jambo ambalo litahatarisha usalama wao.

Serikali ya Tripoli imekanusha kuhusu ukosefu wa usalama kwenye mji huo licha ya kukiri kuwepo kwa makundi ya waislamu wenye msimamo mkali ambao walikuwa wanaiunga mkono Serikali iliyokuwa ikiongozwa na marehemu Muamar Gaddafi.

Mwishoni mwa mwaka jana watu wasiofahamika walivamia ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Benghazi na kuuchoma moto na pia kumuua balozi wake pamoja na maofisa wengine wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.