Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Ufaransa yaendeleza mapambano na waasi nchini Mali, raia 40 wa kigeni watekwa na waasi

Vikosi vya kijeshi vya Ufaransa vimepambana na Waasi nchini Mali wakati Wapiganaji walio na Ushirika na kundi la wanamgambo la Al Qaeda nchini Algeria wamewaua watu wawili na kuwashikilia Mateka Raia wa Kigeni 40.Wanamgambo wa Kiislamu wamesema kuwa wanawashikilia Mateka hao wakiwemo Raia saba wa Marekani baada ya kushambulia Mtambo wa Gesi Mjini Amenas Mashariki mwa Algeria.

REUTERS/Francois Rihouay
Matangazo ya kibiashara

Victoria Nuland ambaye ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa Marekani hapa amethibitisha kukamatwa Mateka kwa Raia wa Marekani.
 

Shambulio hilo limeelezwa kutekelezwa kupinga Operesheni ya kijeshi nchini Mali inayofanywa na Majeshi ya Ufaransa na hatua ya Algeria kufungua anga lake kwa ajili ya Ndege za mashambulizi ya anga za Ufaransa.
 

Mashambulizi yanayofanywa na Ufaransa dhidi ya waislamu wenye msimamo mkali yanalenga kudhoofisha nguvu za waasi hao ambao wameweka katika himaya yao eneo la kaskazini mwa nchi.
 

Katika hatua nyingine Umoja wa Afrika umetangaza kupeleka jeshi nchini Mali kwa ajili ya kusaidia harakati za kukomboa eneo hilo la kaskazini mwa Mali huku waasi hao wakionekana kujipanga kwa ajili ya mapambano.
 

Hata hivyo hatua ya Umoja wa Afrika imekosolewa na wachambuzi wa masuala ya siasa huku wakidai kuwa imekuja ikiwa imechelewa.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.