Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Ufaransa yapeleka wanajeshi 750 Kaskazini mwa Mali kukabiliana na Makundi ya Waislam yenye Msimamo Mkali

Serikali ya Ufaransa imetangaza idadi ya wanajeshi wake ambao wapo kwenye operesheni ya kupambana na Makundi ya Waislam wenye msimamo mkali wanaoshikilia eneo la Kaskazini mwa Mali imefikia mia saba na hamsini huku mpango wao ni kuwa na wanajeshi 2500. Rais wa Ufaransa Francois Hollande ndiye ametangaza idadi hiyo mpya ya wanajeshi ikiwa niongezeko la wanajeshi 250 baadaya hapo awali kupelekwa wanajeshi 500 kwa ajili ya kuisaidia serikali ya bamako kukabiliana na Makundi hayo yanashikilia eneo la Kaskazini tangu kufanyika kwa mapinduzi.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasili Bamako, Mali kuungana na wenzao kwa ajili ya operesheni ya kukabiliana na Wapiganaji wa Kiislam
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasili Bamako, Mali kuungana na wenzao kwa ajili ya operesheni ya kukabiliana na Wapiganaji wa Kiislam REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ufaransa inasema imekwenda Kaskazini mwa Mali kupambana na makundi ya kigaidi sambamba na kuwalinda wananchi wa Ufaransa na wale wa Mali dhidi ya mashambulizi ambayo yamekuwa yakitekeleza na Makundi hayo yakiwemo Ansar Dine na MUJAO.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kupitia wanachama wake wa kudumu kumi na tano wameridhia kuisaidia Ufaransa kwenye operesheni hiyo ya kijeshi na tayari Uingereza imeonesha nia yake ya dhati ya kutoa zana za kijeshi lakini si kupeleka wanajeshi wake.

Mashambulizi ya Ufaransa ambayo yalianza rasmi siku ya jumamosi yamesababisha Wapiganaji wa makundi hayo ya Kiislam kuondoka maeneo waliyokuwa wanayashikilia huku yenyewe yakisema yamefanya hivyo kujipanga kabla ya kurejesha maeneo waliyokuwa wayanashikilia ndani ya himaya yao.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Ledrian amesema hadi sasa hawajaanza kutekeleza mashambulizi ya angani japokuwa ndege zao zipo tayari kusambaratisha ngome za Magaidi hao katika Mji wa Timbuktu.

Ledrian amesema hakuna upinzani wa aina yoyote ambao wamekutana nao hadi sasa na wamekuwa wakisonga mbele kwa utulivu wa hali ya juu huku wakiwa na imani ya kuchukua maeneo yote yanayoshikiliwa na Makundi ya Kiislam.

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa UN Gerard Araud ameliambia Baraza la Usalama ya kwamba mataifa kadhaa ya Afrika yamethibitsha kutuma majeshi yake juma hili kuungana na vikosi vyao huko Mali.

Nigeria imesema wanajeshi wake wataungana na wale wa Ufaransa kipindi hiki ambacho Algeria imefunga mpaka wake na Mali huku Mauritania ikitangaza msimamo wake wa kutongilia kati mgogoro huo.

Naibu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha UPR Mohamed Aldorma akithibitsha uamuzi wa nchi ya Mauritania kutoingilia kati kwa namna yoyote ile mgogoro ambao unaendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa Mali.

Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO nayo imeunga mkono kile kinachoendelea nchini Mali nao kupitia Msemaji wake Oana Lungescu na kukiri hiyo ni hatua nzuri ya kukabiliana na Makundi ya Kigaidi.

Kundi la Wanamgambo lenye maskani yake nchini Afghanistan kupitia Msemaji wake Zabihullah Mujahid limesema hatua hiyo ya uvamizi wa kijeshi si kitu cha kuungwa mkono hata kidogo na inawapasa wanajeshi wa Ufaransa kuondoka mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.