Pata taarifa kuu
ITALIA

Papa Benedicto aomba amani Syria na mataifa yenye vita, katika salamu za Noeli

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto wa XVI ametoa wito wa kukomeshwa kwa umwagaji damu nchini Syria na kutafuta suluhu la kisiasa katika mzozo unaolikumba taifa hilo. 

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto XVII
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto XVII forward.com
Matangazo ya kibiashara

Papa Benedicto ametoa ujumbe huo leo Jumanne wakati wa ibada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya sikukuu ya Noeli iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro wa Basilica,na kutoa ujumbe ambao pia umegusa mataifa mbalimbali duniani yenye vita na migogoro ya kisiasa.

Katika ujumbe huo Papa Benedicto amesema kuwa kuna matumaini duniani hata katika nyakati ngumu zaidi, na kuomba amani izaliwe miongoni mwa watu wa Syria ambao wamejeruhiwa na kugawanywa kwa kiasi kikubwa na mgogoro ambao hauna huruma kwa wasioweza kujitetea na unao gharimu maisha ya wasio na hatia.

Papa amesisitiza kuwa ni lazima umwagaji damu ukomeshwe nchini Syria,na njia za kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani na wenye mahitaji irahisishwe huku akitaka mazungumzo ya muafaka wa kisasa yafanyike ili kumaliza mgogoro huo.

Zaidi ya watu elfu arobaini na nne wameuwawa nchini Syria tangu kuzuka kwa machafuko dhidi ya serikali mnamo mwezi Machi mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.