Pata taarifa kuu
Syria-Machafuko

Maelfu ya wakimbizi wa Kipalestina waliokuwa nchini Syria wakimbia kuokoa maisha yao

Takriban watu elfu kumi na tatu kutoka jamii ya wakimbizi wa kipalestina waliokuwa katika kambi ya Yarmuk nchini Syria wamekimbilia katika eneo la Square one karibu na nchi ya Lebanon. Tangu mwishoni mwa juma lililopita Raia wa Palestina 3000 wamewasili nchini Lebanon wakikimbia mapigano yanayopamba moto nchini Syria.

Reuters/Majed Jaber
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa lililokuwa likiwasaidia Wakimbizi wa Palestina wamesema kuwa Wakimbizi hao hivi sasa wamepanga katika makazi ya hadhi ya chini katika makambi ya 12 ya nchini Lebanon.

Wakiwa nchini Lebanon Raia wa Palestina wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha ikiwemo ukosefu wa ajira na hali duni katika Makambi wanayoishi.

Katika hatua nyingine hapo jana alhamisi Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa UN, liliwekea vikwazo makampuni ya nchini Iran yanayoshutumiwa kuuzia silaha Serikali ya Syria.

Halikadhalika Baraza la Usalama limezuia Mali za Makampuni hayo na kuzuia kufanyika kwa biashara na Makampuni hayo ya Iran.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.