Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Chanjo ya ugonjwa wa polio yasitishwa katika maeneo yote nchini Pakistan

Shirika la umoja wa mataifa UN linalohudumia watoto duniani UNICEF likishirikiana na shirika la afya duniani WHO wameahirisha kampeni za mpango wa kutokomeza ugonjwa wa kupooza au polio nchini Pakistan baada ya mashambulizi dhidi ya watoa huduma kushika kasi na kusababisha vifo vya watu tisa katika kipindi cha siku tatu pekee.

Daniel Berehulak/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mapema leo jumatano watu wenye silaha walifanya mashambulizi kwa wahudumu wa afya waliokuwa wamebeba chanjo za ugonjwa wa polio, suala lililopelekea UNICEF na WHO kusitisha zoezi hilo mara moja.

Msemaji wa UNICEF Michael Coleman ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya mashambulizi ya mjini Karachi na Peshawar lakini kuanzia leo wanasitisha huduma nchi nzima baada ya umwagaji damu kuendelea kushuhudiwa.

Pakistan ni moja kati ya nchi tatu duniani ambazo bado ugonjwa wa polio unaenea kasi kubwa lakini juhudi za kutokomeza ugonjwa huo zimekuwa zikipingwa vikali na wanamgambo wa kundi la Taliban ambao wanadai zoezi hilo linatumiwa kama mwamvuli wa vitendo vya kijasusi.

Idai ya wagonjwa wa polio ilishuka mpaka 28 mwaka 2005 lakini imeongezeka kwa kasi na kufikia 198 mwaka 2011 takwimu ambazo ni kubwa zaidi kufikia katika kipindi cha muongo mmoja suala mbalo linadidimiza juhudi za serikali ya Pakistan na jumuiya za kimataifa katika kutokomeza ugonjwa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.