Pata taarifa kuu
PALESTINA-UN

Palestina kuwasilisha ombi la uanachama Umoja wa Mataifa, Marekani na washirika wapania kupinga

Marekani imeendelea na mpango wake wa kuishinikiza serikali ya Mamlaka ya Palestina kuacha mkakati wake wa kutaka kupatiwa unachama rasmi wa Umoja wa Mataifa UN lakini Rais Mahmud Abbas amesema hawatorudi nyuma kwenye hili.

REUTERS/Alaa Badarneh
Matangazo ya kibiashara

Marekani ikishiriki na Uingereza, Israeli na Italia zote zimekuwa mstari wa mbele kupinga hatua ya Mamlaka ya Palestina kupata uanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa UN huku Ufaransa ikiunga mkono hatua hiyo.

Umoja wa Mataifa UN unatarajia kupiga kura baadaye hii leo kupitisha azimio hilo la kulikubali ombi la Palestina au la na hapa Mkuu wa Tume ambayo inasimamia mchakato huo Hanan Ashrawi amesema watafanikiwa kupata uanachama.

Wachambuzi wa Siasa wanaona huu ni wakati muafaka kwa Mamlaka ya Palestina kupata uanachama huo rasmi wa Umoja wa Mataifa UN.

Nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa UN ndiyo ambao wataamua kama Mamlaka ya Palestina itakuwa mwanachama rasmi wa Umoja huo lakini tayari UNESCO ndiyo shirika pekee linaloitambua nchi hiyo rasmi.

Palestina imekuwa ikipigania uanachama wa UN kwa kipindi kirefu lakini hatua imekuwa ikigonga mwamba kutokana na upinzani mkali ambao umekuwa ukiwekwa na mataifa makubwa yenye kura za turufu.

Kiongozi wa Palestina kwa upande wake amesema wanataka uanachama huo ili uweze kuisadia nchi yao kuwa huru zaidi na hivyo kupanua wigo wa kutafuta suluhu baina yake na Israeli kuhusu eneo la ukanda wa Gaza.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.