Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa mke wa Gbagbo

Mahakama kuu ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC imetowa hati ya kukamatwa kwa Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo ambaye anazuiliwa na mahakama hiyo jijini Hague nchini Uholanzi. 

Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire
Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire mamluks.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Hati hiyo iliandikwa tangu Februari mwaka 2012, na hatimaye kuwekwa bayana jana Alhamisi Novemba 22 mwaka 2012 ambapo Simone Gbagbo anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu uliotekelezwa baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2011.

Chama cha rais wa zamani cha FPI kimelaani hati hiyo ya kimataifa ya kukamatwa kwa Simone Gbagbo mwenye umri wa miaka 63 ambaye anatuhumiwa kushiriki katika mkutano wa kupanga mauaji na ubakaji dhidi ya wafuasi wa rais wa sasa Allasane Dramane Ouattara kati ya Disemba 16 mwaka 2010 hadi April 12 mwaka 2011.

Msemaji wa mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC Fadi El Abdallah amesema kuwa mke wa Gbagbo anatakiwa kutihibitisha kuwa hana hatia.

Kukataa kutoa madaraka kwa rais aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi, kuliitumbukiza nchi hiyo katika lindi la machafuko yaliyo gharimu maisha ya watu wanaoakadiriwa kufikia elfu tatu ambapo kwa sasa Laurent Gbagbo anazuiliwa huko Hegue kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.