Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Rais wa Maurtania kurejea nyumbani Jumamosi hii

Upinzani nchini Mauritania umewataka wananchi wa taifa hilo kuandamana wakidai uundwaji wa utawala wa kipindi cha mpito, ambapo jana jioni katika jiji la Nouakchott maandamano hayo yameshudiwa. 

Rais wa Maurtania Ould Abdel Aziz.
Rais wa Maurtania Ould Abdel Aziz. REUTERS/Darrin Zammit Lupi/Files
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yanajiri baada ya kutangazwa kwa tarehe ya kurejea nchini kwa rais wa taifa hilo Ould Abdel Aziz ambae alijeruhiwa na mwanajeshi wake Ocotba 13 mwaka huu na kulazimika kwenda kupata matibabu zaidi nchini Ufaransa.

Tangu kipindi hicho taifa hilo lenye sifa ya kutokea mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara limekuwa likiongozwa na viongozi wa serikali, huku hali ya usalama ikiendelea kuimarika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.