Pata taarifa kuu
BURMA-MAREKANI

Raisi Barack Obama ziarani Burma ahimiza kuimarishwa kwa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Raisi wa Marekani Barack Obama amesema nchi ya Burma ina safari ndefu katika historia ya mageuzi ambayo yataifikisha mbali nchi hiyo iliyoko kusini mashariki mwa bara la Asia.

Raisi wa Marekani Barack Obama, akiwa na kiongozi wa upinzani nchini Burma na mshindi wa tuzo ya Nobel Aung San Suu Kyi.
Raisi wa Marekani Barack Obama, akiwa na kiongozi wa upinzani nchini Burma na mshindi wa tuzo ya Nobel Aung San Suu Kyi. REUTERS/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa marekani amesema kuwa shauku ya mabadiliko imefikiwa na agenda ya mageuzi na kuongeza kuwa uwepo wake nchini humo ni kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kirafiki baina yao.

Hata hivyo katika hotuba yake raisi Obama akiwa chuo kikuu cha Rangoon amewataka raia wa Burma kukiunga mkono chama cha kiislamu cha Rohingya baada ya kumalizika kwa machafuko ya hivi karibuni.

Umati mkubwa wa raia nchini humo walijitokeza kumlaki raisi Obama huku wakipeperusha bendera ya Marekani na kupanga mistari katika barabara za mitaa mbalimbali.

Ziara ya raisi wa Marekani nchini Burma ililenga kuunga mkono mageuzi yaliyofanywa na serikali ya raisi Thein Sein tangu kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi mnamo mwezi November 2010.

Wanaharakati wameonya kuwa ziara hiyo huenda imekuwa ya mapema sana wakati bado masuala kadhaa hayajatafutiwa ufumbuzi ikiwemo wafungwa wa kisiasa, migogoro ya kikabila katika maeneo ya mpakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.