Pata taarifa kuu
SYRIA

Nchi za Kiarabu zaunga mkono Baraza la Mapinduzi Syria

Umoja wa nchi za Kiarabu hatimaye umetangaza rasmi kuutambua muungano mpya wa baraza la mapinduzi nchini Syria SNC na kwamba itashirikiana nao katika kuhakikisha wanafikia malengo yao.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mara baada ya kikao cha mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja huo, waziri mkuu wa Qatar Sheikh Hamad Bin Jassem al-Thani amesema kuwa umoja huo sasa utalitambua baraza la SNC kama chombo halali kinachopigania maslahi ya watu wa Syria.

Kauli ya viongozi wa umoja huo inakuja saa chache mara baada ya siku ya jumapili viongozi mbalimbali wanaounda makundi yanayopigana nchini Syria kukubaliana na kumteua Mouaz al-Khatibu kama mwenyekiti mmoya wa muungano wa makundi ya waasi nchini Syria.

Viongozi hao wametaka umoja huo kupewa ushirikiano wa kutosha ikiwemo kupatiwa vifaa vya kijeshi vya kisasa ili kuweza kukabiliana na nguvu ya majeshi ya Syria ambayo yanatumia zana za kisasa na zenye nguvu.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo bado wanaona kuwa SNC ina safari ndefu katika kufikia malengo yake kwakuwa bado kuna mgawanyiko ndani ya wajumbe wake lakini kwa nchi zinazounga mkono mapinduzi nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.