Pata taarifa kuu
ISRELI-PALESTINA-UN

Kiongozi wa Palestina aweka msimamo kuhusu uanachama kwenye Baraza la Usalama la UN

Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas ameendelea kusisitiza kauli yake ya kwamba Palestina itawasilisha rasmi ombi lake la kuwa mwanachama wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa huyo amesema kuwa watawasilisha ombi hilo tarehe 29 ya mwezi huu licha ya upinzani kutoka kwa nchi ya Marekani na Israeli.

Akizungumza kwenye kikao cha jumuiya ya nchi za Kiarabu kinachoendelea mjini Cairo Misri, Abbas amezitaka nchi hizo kuunga mkono hatua yake na kuhakikisha inapatiwa uanachama wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameendela kusisitiza nchi yake kujilinda dhidi ya uvamizi wowote toka kwa nchi ya palestina na washirika wake.

Wakati Palestina ikijiandaa kuwasilisha ombi hilo tayari nchi za Marekani na Israel zimeeleza wazi kutounga mkono azimio hilo na kwamba italiwekea ngumu wakati suala hilo litakapojadiliwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.