Pata taarifa kuu
SYRIA-QATAR

Viongozi wa upinzani nchini Syria waendeleza mikakati ya kumwondoa rais Assad madarakani

Viongozi wa upinzani nchini Syria wanakutana katika mkutano wao unaofanyika Qatar wakiwa na lengo la kuendelea na mkakati wa kuuangusha utawala wa rais Bashar Al Assad pamoja na kufanya uchaguzi wa viongozi wake ambao wataongoza mchakato huo. 

Viongozi wa upinzani na marafiki wa Syria
Viongozi wa upinzani na marafiki wa Syria washingtonpost.com
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu ambao unahudhuriwa pia na wanaojiita marafiki wa Syria kutokana na kujipambanua kuwasaidia wapinzani inatajwa kama sehemu moja wapo ya juhudi za kufikia malengo ya kuichukua nchi hiyo.

Mwanasiasa machachari katika kambi ya upinzani kutoka Baraza la Taifa la Syria SNC Riad Seif amewaambia wanahabari mapema kwamba nia ya upinzani ni kuhakikisha inakuwa na viongozi bora kuongoaza nchi hiyo.

Kwa upande wake rais Assad amejibu kauli iliyotolewa na jumuiya ya nchi za kiarabu ya kwamba muda wake unahesabika kwa kusema hawezi kuondoka madarakani na yupo tayari kufa ndani ya Syria .

Wapiganaji wa upinzani nchini Syria wameanza kuingia kwenye lawama za kutekeleza ukiukwaji wa haki za binadamu kutokana na video kuonesha wakiwapiga risasi wafuasi wa rais Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.