Pata taarifa kuu
MALI

Harakati za uvamizi wa kijeshi nchini Mali zashika kasi

Viongozi wa nchi za Magharibi mwa Afrika wamezidisha juhudi za maandalizi ya Jeshi ambalo litapelekwa Kaskazini mwa Mali kwa lengo la kupambana na makundi ya Waislam wenye msimamo mkali huku wakisubiri ridhaa ya Umoja wa Mataifa UN. 

Viongozi wa ECOWAS
Viongozi wa ECOWAS portaltoafrica.com
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao chini ya mwamvuli wa jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutumia Jeshi kukabiliana na Ansar Dine, MUJAO na AQIM ambao wanaelezwa kufanya uharibifu mkubwa huko Timbuktu.

Kundi la Ansar Dine kupitia msemaji wake Mohamed Ag Aharid limetoa onyo kwa mpatanishi wa mgogoro huo rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kama jeshi litatumika basi eneo hilo lote litakuwa kwenye hali mbaya.

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika ukanda wa Sahel Romano Prodi amesema kuwa hiyo ni hatua ya mwisho baada ya mazungumzo na rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.