Pata taarifa kuu
SOMALIA

Shambulio nje ya bunge laua mmoja Somalia.

Mlipuko mkubwa unaoaminika kuwa wa bomu lililokuwa limetegwa garini,umesikika nje ya ukumbi wa bunge nchini Somalia na kusababisha kifo cha mtu mmoja. 

Wakazi wakimbeba mmoja wa majeruhi katika shambulio la hivi karibuni nchini Somalia.
Wakazi wakimbeba mmoja wa majeruhi katika shambulio la hivi karibuni nchini Somalia. uk.reuters.com
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo ni la karibuni katika mfululizo wa mashambulizi katika mji mkuu wa nchi hiyo ambapo baada ya kusikika kwa mlipuko huo maafisa wa usalama wakiwa wamevalia sare za kijeshi walionekana wakielekea eneo la tukio.

Hata hivyo hakuna kundi lolote hadi sasa ambalo linadaiwa kutekeleza shambulio hilo ingawa kundi la Al Shabab,lenye uhusiano na wanamgambo wa Al Qaeda limefanya mashambulizi kadhaa ya msituni katika mji mkuu Mogadishu tangu mwaka jana.

Mapema wiki hii kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al-Zawahiri amewataka waislam kuunga mkono wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia ambao kwa miezi ya hivi karibuni wamerudishwa nyuma a askari wa umoja wa Afrika kwa kuwanyang'anya udhibiti wa ngome zao kadhaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.