Pata taarifa kuu
SYRIA

Baraza la upinzani nchini Syria wakutana nchini Qatar kujadili namna ya kujiimarisha.

Baraza la Taifa la upinzani nchini Syria , linakutana Doha nchini Qatar kupanua uanachama wake, huku ikiripotiwa kuwa kundi hilo linadhamiria kulinda jukumu lake la kuongoza kwa namna yoyote ile. 

Wajumbe wa baraza la upinzani nchini Syria.
Wajumbe wa baraza la upinzani nchini Syria. euronews.com
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa baraza hilo la SNC Abdel Basset Sayda pia ameshutumu kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ya kukomesha mauaji yanayofanywa na vikosi vinavyounga mkono serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Matamshi yake ameyatoa wakati wa mkutano wa wajumbe wa baraza hilo SNC katika mji mkuu wa Qatar Doha, wakati huu ambapo Marekani inatoa shinikizo kwa upinzani kutengeneza muundo mpana wa baraza hilo.

Sayda amesema kuwa SNC itashiriki katika mkutano mkubwa wa upinzani siku ya Alhamisi ulioitishwa na mwenyeji Qatar na Umoja wa mataifa ya Kiarabu, lakini amesisitiza kuhusu jukumu la uongozi la baraza hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.