Pata taarifa kuu
ATHENS-UGIRIKI

Mgomo wa wiki nzima waanza nchini Ugiriki kupinga mpango wa kubana matumizi

Huduma za usafirishaji wa uma na wafanyakazi wa Vyombo vya habari nchini Ugiriki wameanzisha mgomo wa wiki nzima kwa lengo la kupinga mpango wa kubana matumizi ambayo ni masharti kutoka kwa wakopeshaji, mpango ambao unatarajiwa kuwasilishwa bungeni.

Raia wa Ugiriki wakiwa katika maandamano kupinga mabadiliko yanayotekelezwa na serikali yao.
Raia wa Ugiriki wakiwa katika maandamano kupinga mabadiliko yanayotekelezwa na serikali yao. Reuters/Yorgos Karahalis
Matangazo ya kibiashara

Usafiri wa Treni jijini Athens na Madereva taxi nchini humo walisitisha huduma hali iliyosababisha kuwepo kwa Msururu wa Magari mjini, halikadhalika waandishi wa vyombo vya habari nchini humo, Magazeti, Redio na Televisheni wamefanya mgomo wa saa 24.

Huduma za hospitalini nazo zimeonekana kudorora huku wafanyakazi wachache wakijitokeza kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kila siku.

Umoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umeme la Umma pia limetangaza mgomo mpaya wa Saa 48 kuanzia jumatatu jioni, huku mgomo huo ukitarajiwa kuwa mkubwa zaidi siku ya Kesho na Jumatano kufuatia wito wa Chama cha wafanyakazi wa Uma na Binafsi kuitisha mgomo Nchi nzima.

Mpango huu mpya wa Kubana Matumizi unagusa Mishahara, punguzo kwenye Malipo ya Wastaafu, na kupunguza wafanyakazi.

Ugiriki imelazimika kufikia hatua hiyo ili kupata mkopo wa Euro Bilioni 31.5 kutoka Umoja wa Ulaya, Shirika la Fedha duniani, IMF na Benki kuu ya ulaya, ili kuepuka taifa hilo kuingia Mufilis katikati ya Mwezi huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.