Pata taarifa kuu
MALI

Wapatanishi wakuu wa mgogoro wa Mali kujaribu kushawishi kundi la Ansar Dine kukata mahusiano na Al Qaeda

Wapatanishi wakuu wa mgogoro wa Mali wamesema kuwa watajaribu kushawishi moja ya vikundi vya Kiislam vinavyo dhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, kukata mahusiano na tawi Al-Qaeda la Afrika Kaskazini, afisa mmoja amesema jana Jumamosi, baada ya gazeti la Algeria kuripoti kuwa kundi hilo linafikiria kufanya hivyo.

Djibril Bassolé waziri wa kigeni wa Burkina -Faso
Djibril Bassolé waziri wa kigeni wa Burkina -Faso Reuters/Mohamed Nureldin
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Djibrill Bassole, ambaye anasaidia jitihada za upatanishi za nchi yake kukomesha mgogoro wa miezi saba wa nchi jirani ya Mali , amesema anapanga kukutana na wawakilishi kutoka Ansar Dine mwishoni mwa wiki hii.

Siku ya Ijumaa kundi la Ansar Dine lilipeleka ujumbe nchini Algeria na Burkina Faso kwa mazungumzo ya amani.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.