Pata taarifa kuu
MYANMAR

Umoja wa Mataifa UN wataka mapigano ya kidini nchini Myanmar yamalizwe mara moja kipindi hiki ambacho maelfu wamekimbia makazi yao

Umoja wa Mataifa UN umetaka hatua za haraka zichukuliwe ili kukabiliana na machafuko ambayo yamechangia vifo vya mamia ya raia nchini Myanmar katika Jimbo la Rakhine huku wengine maelfu wakilazimika kuyakimbia makazi yao.

Wananchi ambao wamekimbia makazi yao katika Jimbo la Rakhine nchini Myanmar kutokana na kuzuka kwa mapigano
Wananchi ambao wamekimbia makazi yao katika Jimbo la Rakhine nchini Myanmar kutokana na kuzuka kwa mapigano
Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya kidini yameendelea kushuhudiwa nchini Myanmar na takwimu za serikali zinaonesha watu elfu ishirini na mbili na mia tano wamekimbia makazi yao huku nyuma elfu nne na mia sita zikichomwa moto.

Umoja wa Mataifa UN umesema timu maalum ambayo inaongozwa na Ashok Nigam itaelekea katika Jimbo la Rakhire kijionea madhara ambayo yametokea kutokana na mapigano ya kidini yanyoendelea.

Vikosi vya serikali vimepelekwa katika Jimbo la Rakhine lakini bado kumeendelea kushuhudiwa mapigano baina ya waumini wa kiislam wa Rohingya dhidi ya wale wanaoamini kupitia Budha.

Mapigano hayo ya kidini yalizuka mnamo tarehe 21 ya mwezi Oktoba mwaka huu na hali imezidi kuwa mbaya kila uchao huku kila upande ukiendelea kujihami kwa silaha na kuwashambulia wenzao.

Ghasia hizo zilianza pale ambapo wauamini wa Kiislam walipowatuhumu Mabudha kutokana na kutekeleza ubakaji huku wao wakiwatuhumu wenzao kwa kumuua mwanamke ambaye amaamini kwenye imani yao.

Wito huu wa kumaliza kwa machafuko unatolewa kipindi hiki ambacho mkuu wa Timu inayoenda kujionea hali ilivyo Jimboni Rakhine chini ya Nigam ikitoa taarifa ya kuonesha kuumizwa na mauaji ambayo yanendelea.

Silaha za kijadi ndizo zimekuwa zikitumika zaidi kwenye mapigano hayo na hivyo kuendelea kushuhudia watoto na wanawake wakiendelea kuathiriwa na mapigano hayo ya kidini ambayo yalianza kuonekana mwezi Juni.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.