Pata taarifa kuu
IRAN-MASHARIKI YA KATI

Ban Ki Moon aunga mkono mkutano wa kuzungumzia silaha za nyuklia Mashariki ya Kati

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ameunga mkono mkutano unaolenga kuzungumzia masuala ya Silaha za Nuklia mashariki ya kati, akitoa wito wa nchi zote katika ukanda huo kuhudhuria.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Finland iko tayari kuhodhi mkutano huo jijini Helsinki katikati ya mwezi Desemba, hatua iliyosifiwa na Ban kuwa ni Fursa ya kipekee kwa mataifa yote kwa Pamoja kujadili mustakabali wa usalama wa nchi zao.

Ban ki moon amekaribisha pia jumuia ya mataif aya kiarabu kuangalia namna ya kuweza kushiriki katika mkutano huo katika mtazamo wa kujenga zaidi.

Katibu Mkuu huyo pia ameunga mkono namna ambavyo nchi za kiarabu zinalichukulia kwa umakini suala la mkutano huo kwa lengo la kujenga na sikubomoa.

Nchi ya Islael na washirika wake nchi za magharibi wanahofia kuwa Iran inaendesha mpango wa nyuklia kwa ajili ya kutengeneza silaha za maangamizi wakati Iran imeendelea kukanusha na kwamba mpango wake wa nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Si Israel wala Iran zilizoahidi kushiriki mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.