Pata taarifa kuu
Syria-Uturuki

Uturuki yalazimisha ndege Syria kutua kwa kuhofia silaha za maangamizi

Serikali ya Uturuki imezuia baadhi ya mizigo kutoka ndege ya shirika la Syria iliyokuwa inatokea urusi kuelekea Damascus ambapo inavichunguza vifaa ambavyo vilikuwa vimebebwa na ndege hiyo.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya uturuki imekuja kufuatia siku ya Jumatano usiku kuamrisha marubani wa ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa Ankara kwa madai kuwa wamepokea taarifa kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba mizigo ambayo inahofiwa kuwa ni vifaa vya makombora.
 

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Ahmet Davotoglu amesema kuwa serikali yake ililazimika kuamuru ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa Ankara.
 

Waziri huyo alisema, baada ya kupokea taarifa za siri kuwa kulikuwa na mizigo ambayo huenda ikawa ni vifaa vya mawasiliano ambavyo vingetumika kwenye makombora ya masafa marefu ndiyo waliamua kuchukua hatua hiyo.

Hata hivyo mara baada ya kushusha vifurushi hivyo mamlaka nchini humo ziliiruhusu ndege hiyo kuruka kuendelea na safari yake wakati maofisa wa jeshi la nchi hiyo wakifanyia uchunguzi vifaa ambavyo wamevikamata.

Katika hatua nyingine nchi hiyo imetangaza anga ya Syria kutokuwa salama na kuzitaka ndege zake zote kutopita kwenye anga yake.

Uturuki imezsema kwamba haitasita kwa mara nyingine kulazimisha ndege ya Syria kutua kwenye uwanja wake iwapo itatumia anga yake.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.