Pata taarifa kuu
ULAYA-UGIRIKI

Sera za Ujerumani za kubana matumizi Ulaya zakosolewa

Maelfu ya wananchi wameandamana nchini Ugiriki nje ya ukumbi ambao kansela wa Ujerumani Angela Markel alikuwa anakutana na mwenyeji wake waziri mkuu Antonio Samaras wakipinga ziara ya kiongozi huyo nchini mwao.

REUTERS/Thanassis Stavrakis
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walijitokeza kuunga mkono maandamano hayo ya wananchi waliokua wakipinga sera za Ujerumani kuhusu Ulaya.

Wananchi hao waliokuwa wakiandamana wamekosoa hatua ya nchi ya Ujerumani kuwa kinara katika kushinikiza mataifa ya Ulaya kutekeleza mpango wa ubanaji matumizi.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji hao ambapo pia watu kadhaa walikamatwa kuhusiana na maandamano hayo.

Mandamano hayo yanakuja huku kukiwa na jitihada mbalimbali za kukabiliana na mdororo wa uchumi katika nchi za Ulaya na hata kulazimika kupitisha sera ya kubana matumizi kwa nchi husika.

Suala linaloyumbisha nchi hizo ni pamoja na kukabiliwa na madeni yaliyotokana na kukopa fedha kwa ajili ya kukabiliana na hali ya kuyumba kwa uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.