Pata taarifa kuu
Syria

Majeshi ya waasi wa Syria yadaiwa kushika maeneo muhimu, NATO kuisadia Uturuki kijeshi

Waasi nchini Syria wamefanikiwa kuushikilia maeneo muhimu kwenye mji wa Allepo hatua inayoelezwa kuwa ni pigo kwa vikosi vya serikali ambavyo vimekuwa vikijaribu kuurejesha kwenye hiamaya yake mji wa Aleppo.

REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Kusonga mbele kwa waasi na kuingia mji wa Maaret al-Numan kumekuja baada ya kutekelezwa kwa mashambulizi mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga mjini Damascus hali iliyolazimu vikosi vya rais Asad kuimarisha ulinzi zaidi kwenye mji wa Damascus na kutoa mwanya kwa waasi kusonga mbele.

Wakati huohuo Serikali ya Uturuki kwa mara nyingine imeionya serikali ya Syria kuwa haitasita kulipiza kisasi dhidi ya shambulio lolote ambalo litafanywa na vikosi vya Serikali kwenye maeneo ya mpaka wake.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Jumuiya ya majeshi ya nchi za magharibi za kujihami NATO Anders Fogh Rasmussen amesema kuwa jumuiya hiyo imejipanga kuisaidia nchi ya Uturuki katika kuipatia ulinzi ikiwemo kutumia nguvu za kijeshi.

Kufuatia mashambulizi yanayoendelea katika mipaka ya Syria na Uturuki kumezuka hisia kuwa huenda nchi hizo zikaingia katika vita hali ambayo inaweza kuondoa matumaini ya kusaka suluhu ya mgogoro wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.