Pata taarifa kuu
MALI-UN

Viongozi wa Mali wajiandaa kuwaondoa waasi wa kiislam Kaskazini mwa nchi hiyo.

Viongozi nchini Mali wanajiandaa kwa vita ya kuwaondoa wakazi wa eneo la Kaskazini mikononi mwa makundi ya waasi wa Kiislam, mpango ambao umekuja baada ya mkutano wa umoja wa mataifa UN, licha ya mashaka ya baadhi ya majirani zake kuhusu kikosi kazi cha kimataifa. 

Rais wa mpito wa  Mali, Dioncounda Traore.
Rais wa mpito wa Mali, Dioncounda Traore. AFP/Habibou Kouyaté
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na rais Dioncunda Traore, viongozi hao wanasema kuwa wameona ahadi ya mshikamano kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ikiwa upande wao hivyo wanaamini watafanikiwa kulikomboa eneo la Kaskazini.

Aidha chanzo hicho kimeongeza kuwa Serikali ya mali ilijua kwamba majirani zake hasa Algeria walikuwa wakijaribu kutengeneza sababu kwa ushirikiano na Mauritania na Niger kupinga kupelekwa kwa vikosi vya kigeni nchini Mali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.