Pata taarifa kuu
ATHENS-UGIRIKI

Vyama vya wafanyakazi nchini Ugiriki vyaitisha mgomo wa nchi nzima kupinga sera ya ubanaji matumizi

Vyama vya wafanyakazi nchini Ugiriki hii leo kwa mara ya kwanza vimeitisha mgomo wa nchi nzima utakaodumu kwa saa ishirini na 24 kupinga hatua ya Serikali kutangaza mpango zaidi wa kubana matumizi.

Moja ya maandamano ya wafanyakazi nchini Ugiriki
Moja ya maandamano ya wafanyakazi nchini Ugiriki Reuters/Yorgos Karahalis
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huo ambao unaitishwa ikiwa ni miezi michache imepita toka kuingia madarakani kwa Serikali ya muungano wa vyama vya Conservative, unakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Serikali mpya kushughulikia mzozo wa kiuchumi.

Mgomo huo ulioitishwa hii leo unapinga mpango mpya wa Serikali iliyoutangaza wa kubana matumizi ya bajeti yake kwa kiasi cha Euro bilioni 11.5.

Toka nchi hiyo imeanza mpango wa ubanaji matumizi kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira jambo ambalo limeamsha hasira kwa wananchi na wafanyakazi ambao wamepoteza kazi zao kutokana na mpango wa ubanaji matumizi.

Serikali ya waziri mkuu Antonis Samaras imetangaza pia kutaka kufanyia mabadiliko sera ya mafao na kutaka kuongeza muda wa kustaafu mpaka kufikia umri wa miaka sitini na saba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.