Pata taarifa kuu
PAKISTAN-MAREKANI

Watu 9 wamepoteza maisha nchini Pakistan kwenye maandamano ya kupinga filamu inayodhalilisha Uislam

Watu tisa wamepoteza maisha na wengine zaidi ya themanini wamejeruhiwa kwenye maandamano yakupinga filamu inayomdhalilisha Kiongozi wa Waislam Duniani Mtume Muhammada SWA yaliyoanfaliwa nchini Pakistan. Vifo hivyo vimechangiwa na kuzuka kwa machafuko baada ya maandamano ya amani yaliyopata baraka za serikali ambapo maelfu ya waumini wa Kiislam walijitokeza kuonesha hasira zao kwa Marekani iliyotengeneza filamu hiyo.

Waandamanaji nchini Pakistan wakiwa kwenye maandamano yao baada ya sarat Ijumaa kupinga filamu inayodhalilisha Uislam
Waandamanaji nchini Pakistan wakiwa kwenye maandamano yao baada ya sarat Ijumaa kupinga filamu inayodhalilisha Uislam REUTERS/Mian Khursheed
Matangazo ya kibiashara

Mashuhuda wamesema zaidi ya watu elfu arobaini na tano wamejumuika kwenye maandamano hayo katika Jiji la Karachi huku wakichoma bendera na kubeba mabango ya kulaani kile ambacho kimefanywa na Marekani.

Miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na askari mmoja aliyepoteza maisha katika Jiji la Karachi wakati anakabiliana na waandamanaji waliokuwa na hasira wakitaka kuharibu maslahi za Marekani.

Maandamano hayo yalipata baraka kutoka kwa serikali ya Pakistan ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Hina Rabbani Khar aliwataka waandamanaji wafanye maandamano yao kwa amani bila ya kutekeleza uharibifu.

Serikali ya Marekani ililazimika kukilipa kituo cha Televisheni cha Pakistan kuonesha tangazo la Rais Barack Obama ambalo linamuonesha akilaani filamu hiyo inayodhalilisha Uislam na Kiongozi wao Duniani.

Maandamano ya kupinga filamu hiyo yameshuhudiwa kwenye nchi karibu zote zenye dola ya kiislam ambapo wengi wameendelea kulaani kile ambacho kimefanywa juu ya dhihaka kwa Uislam duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.