Pata taarifa kuu
MAREKANI-PAKISTAN-LEBANON-AFGHANISTAN

Maandamano yaendelea kupinga filamu iliyotengenezwa Marekani ikimdhihaki Mtume Muhammad SAW na Uislam

Maandamano zaidi yanaendelea kushuhudiwa duniani kupinga filamu ya Marekani ambayo inamdhihaki Mtume Muhammad SAW pamoja na Uislam kitu ambacho kimechangia hasira kubwa kwa waumini wa dini hiyo ambayo wamejitokeza kuandamana na hata kushambulia Balozi za Marekani.

Maandamano zaidi yaendelea kupinga filamu iliyotengenezwa Marekani ikimdhihaki Mtume Muhammad SAW
Maandamano zaidi yaendelea kupinga filamu iliyotengenezwa Marekani ikimdhihaki Mtume Muhammad SAW
Matangazo ya kibiashara

Nchi ambazo zimeendelea kushuhudia maandamano hayo ni pamoja na Pakistan, Afghanistan, Ufilipino na Lebanon ambapo maelfu ya waumini wa kiislam wameendelea na maandamano yao ya kuonesha hasira walizonazo juu ya filamu hiyo iliyotengenezwa nchini Marekani.

Hadi kufika sasa mtu mmoja amepoteza maisha kwenye muendelezo wa maandamano hayo ambayo yamekuwa yakienda sambamba na kushambuliwa kwa balozi za Marekani na uchomaji wa bendera za nchi hiyo katika mataifa hayo.

Chanzo cha maandamano hayo yalikuwa nchini Libya ambako Balozi wa Marekani aliuwa na kisha kuendelea katika nchi jirani ya Misri kabla ya kufika Tunisia na Sudan ambako balozi za Marekani zilikuwa matatani.

Marekani kupitia Waziri wa Ulinzi Leon Panetta ameendelea kushikilia msimamo wake hawatokuwa tayari kupeleka vikosi vyao katika nchi hizo kwa lengo la kulinda balozi hizo kwani hilo ni jukumu la nchi husika.

Kiongozi wa Waislam nchini Lebanon Sheikh Nassan Hasrallah ametangaza kuendelea kwa maandamano nchini humo ambapo Kundi la Hezbollah lenyewe limeendelea kuwa mshiriki mkuu.

Kushiriki kwa Hezbollah kunaonekana kama kitisho nchini Lebanon lakini Waziri Mambo ya Ndani Marwan Charbel kutoa hakikisho kwa Washington kwamba wataendelea kulinda mali zote za nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.