Pata taarifa kuu
Syria-machafuko

Lakhtar Brahimi msuluhishi katika mgogoro ataraji kukutana na upande wa upinzani baada ya kujadiliana na wajumbe wa serikali

Msuluhishi wa Mgogoro wa Syria Lakhdar Brahimi anatarajiwa kukutana na Upande wa Upinzani baadaye hii leo baada ya kikao na Viongozi wa serikali lakini amekiri hali inazidi kuwa mbaya katika taifa hilo baada ya miezi kumi na minane ya machafuko.

Lakhdar Brahimi (kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa Syria Woualid al-Mouallem Septemba  13 jijini Damascus.
Lakhdar Brahimi (kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa Syria Woualid al-Mouallem Septemba 13 jijini Damascus. REUTERS/Khaled al-Hariri
Matangazo ya kibiashara

Brahimi ambaye amechukua nafasi ya Kofi Annan aliyejitoa kutokana na kukosa ushirikiano amesema ndugu wa Syria wameingia kwenye mgogoro mkubwa sana ambao ni lazima upatiwe suluhu haraka iwezekanavyo.

Ziara ya Brahimi imekuja huku Waasi wakisema wamesonga mbele huko Aleppo ambapo wanaharakati wameshuhudia watu kumi na moja wakipoteza maisha na hapa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon anataka pande zinazokinzana kuuafikiana.

Mapigano baina ya Jeshi la Serikali na Waasi yameendelea na kuchangia vifo vya raia wengi wasio na hatia kitu ambacho kimekuwa kikigusa Jumuiya ya Kimataifa ambayo hata hivyo imeshindwa kusaidia kukomeshwa kwa machafuko nchini humo.

wakati hayo yakiendelea, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian akiwa ziarani nchini Liban amewaambia waandishi wa habari kwamba nchi yake haina mpango wa kuwapa silaha waasi wanaopambana na serikali ya Assad.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.