Pata taarifa kuu
Ethiopia

Mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu Ethiopia,Meles Zenawi kufanyika leo

Ethiopia inatarajia kuuzika leo mwili wa kiongozi wake aliyehudumu kama waziri mkuu kwa muda mrefu nchini humo Meles Zenawi katika mazishi ya kitaifa.

Baadhi ya waombolezaji nchini Ethiopia wamejitokeza kuomboleza msiba wa Hayati Meles Zenawi,aliyekuwa waziri mkuu nchini Ethiopia
Baadhi ya waombolezaji nchini Ethiopia wamejitokeza kuomboleza msiba wa Hayati Meles Zenawi,aliyekuwa waziri mkuu nchini Ethiopia AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi kadhaa za Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo huku tayari wawakilishi kutoka mataifa ya kigeni wakiwasili Ethiopia jumamosi na kutia sahihi zao katika kitabu cha maombolezo.

Raisi wa Rwanda Paul Kagame na Boni Yayi, wa Benin, ni miongoni mwa viongozi wa Afrika waliowasili mapema katika shughuli za mazishi wa Meles Zenawi.

Raisi wa Benin Boni Yayi ameeelezea kifo cha Zenawi kimeacha pengo kubwa sio tu kwa Ethiopia bali kwa kwa bara zima la Afrika kwa sababu ya maono ya kiongozi huyo na kuunga mkono harakati za kutetea uafrika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.