Pata taarifa kuu
GAMBIA

Gambia yatetea adhabu ya kifo kwa wafungwa.

Gambia imetetea mpango wake wa kuwahukumu kifo wafungwa 9 kwa kuwafyatulia Risasi kufuatia hatua ya Umoja wa Mataifa kukemea kitendo hicho. 

avert.org
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza walielezwa na serikali ya Gambia kuwa hakuna sheria zilizo sahihi kwa asilimia miamoja duniani kote ikiwemo za nchi zao.

Mkuu wa ofisi inayoshughulikia maswala ya haki za binaadamu ndani ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay alisema kuwa kitendo cha Gambia kuidhinisha utekelezwaji wa adhabu ya kifo kwa wafungwa hao ni ukiukwaji wa haki za bainaadamu.

Wafungwa wengine 38 wanaokabiliwa na adhabu ya kifo watapigwa risasi majuma kadhaa yajayo baada ya rais wa Gambia, Yahya Jammeh kutoa amri hiyo ambayo ameahidi kuitekeleza katikati ya mwezi ujao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.