Pata taarifa kuu
NIGERIA

Nigeria yafanya mazungumzo na wawakilishi wa Boko Haram

Serikali ya Nigeria imefanya mazungumzo na wawakilishi wa kundi la kiislam la Boko Haram kwa nia ya kumaliza uasi ambao umesababisha vifo kwa mamia ya watu nchini humo.

Kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wanaofanya uasi Nigeria
Kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wanaofanya uasi Nigeria AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Rais, Reuben Abati amewaambia wanahabari kuwa Mazungumzo hayo kupitia wawakilishi yanatumika ili kuweza kufahamu madai yao na namna ya kufanya kutatua mgogoro huo.

Kauli ya Abati ni ya kwanza ya uthibitisho wa Serikali kufanya mazungumzo hayo kupitia kwa Waziri wa Habari mazungumzo yanayoashiria kuelekea kufanyika kwa Mazungumzo yaliyo Rasmi.

Kundi la Boko Haram linashutumiwa kuua zaidi ya watu 1400 kaskazini na katikati mwa nchi hiyo tangu mwaka 2010.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.