Pata taarifa kuu
cote d'Ivoire

Waziri wa zamani Cote D' Ivoire ashikiliwa na wanausalama

Vyombo vya usalama nchini Cote d' Ivoire vimemuweka kizuizini waziri wa zamani nchini humo Alphonse Douati,mtu muhimu katika chama cha raisi wa zamani Laurent Gbagbo ikiwa ni masaa machache baada ya shambulizi kutokea katika ofisi za chama cha IPF.

Waziri wa zamani nchini Cote D'Ivoire,Alphonse Douat ambaye anashaikiliwa na wanausalama nchini humo.
Waziri wa zamani nchini Cote D'Ivoire,Alphonse Douat ambaye anashaikiliwa na wanausalama nchini humo. news.abidjan.net
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa vyombo vya usalama nchini humo Mamadou Frank Bamba amethibitisha kwamba Douati,ambaye kwa sasa ni kaimu katibu mkuu wa chama cha IPF ameshikiliwa na wanausalama kwa mahojiano zaidi ambapo zoezi hilo litafanyika katika ofisi za usalama nchini humo.

Hata hivyo sababu hasa ya kumuweka kizuizini kiongozi huyo wa IPF haijawekwa wazi.

Hayo yanajiri kufuatia kushambuliwa kwa Makao makuu ya chama cha raisi wa zamani wa Cote d' Ivoire Laurent Gbagbo na kundi la watu wenye silaha na kujeruhi watu watatu huku wawili wakitoroshwa,na kushuhudia lawama zikielekezwa kwa wafuasi wa raisi Ouattara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.