Pata taarifa kuu
HAGUE

Kesi ya Jean Pierre Bemba yaanza Kusikilizwa katika mahakama ya ICC jijini Hague nchini Uholanzi

Kesi ya mauaji na visa vya ukiukwaji wa haki biandamu dhidi ya aliyekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba imeanza katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Mawakili wanaomtetea Bemba wameaza kutoa utetezi wao mbele ya majaji wa Mahakama hiyo wakiongozwa na Jaji Sylvia Steiner.

Bemba mwenye umri wa miaka 49 anakabiliwa na mashtaka matatu, yakiwemo ya ukiukaji wa haki za binadamu yaliyowafanywa na majeshi yake ya kibinafsi katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2002 na 2003.

Majeshi ya Bemba yaliayofahamika kama MLC yanatuhumiwa kutekeleza mauji na mashambulizi dhidi ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati alipoyatuma kwenda kusaidia kupambana na majeshi ya nchi huyo yaliyokuwa yanampindua rais Ange-Felix Patasse.

Mawakili wa Bemba wanasema mteja wao hana makosa na wanadai kuwa mauji yaliyotokea yalikuwa chini ya jeshi la nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kesi dhidi ya Bemba inatazamiwa kumaliza mwezi Machi mwaka ujao.

Mashahidi 59 wanatarajiwa kushiriki katika kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.