Pata taarifa kuu
IRAN-SYRIA

Tehran yaandaa mkutano wa nchi 29 marafiki wa Syria ambao hawaungi mkono vikwazo dhidi ya Syria

Nchi ya Iran hii leo imeandaa mkutano wa mataifa ishirini na tisa marafiki wa Syria, mkutano unaolenga kutafuta suluhu ya mgogoro wa Syria na kusitishwa kwa umwagaji damu nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid al-Moallem (Kushoto) akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Iran  Ali Akbar Salehi(kulia)
Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid al-Moallem (Kushoto) akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Iran Ali Akbar Salehi(kulia) Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ameongeza kuwa nchi yake imetuma ujumbe maalumu wa mashirika ya kutoa msaada nchini humo kwaajili ya kusaidia huduma za kibanadamu kwa raia abao wameendelea kunaswa kwenye mapigano.

Mataifa ambayo hayakujumuishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na mataifa ya Magharibi na zile za Umoja wa nchi za Kiarabu ambazo zinaunga mkono vikwazo ilivyowekewa nchi ya Syria.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, waziri Salehi amesema kuwa kutokana na vikwazo ambavyo vimewekwa kwa nchi ya Syria vimeendelea kuwafanya wananchi wake kukumbana na shida na hali mbaya ya maisha kutokana na kukosekana kwa misaada muhimu.

Iran pia imeyatuhumu mataifa ya magharibi na baadhi ya mataifa ya nchi za Kiarabu kwa kuwafadhili waasi kwa silaha kwa lengo la kuendeleza machafuko nchini humo.

Miongozni mwa mawaziri wa mambo ya nje waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wa Iraq, Pakistan na Zimbabwe.

Nchi ambazo zimetuma mabalozi wake ni pamoja na, Afghanistan, Algeria, Armenia, Benin, Belarus, China, Cuba, Ecuador, Georgia, India, Indonesia, Jordan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Maldives, Mauritania, Nicaragua, Oman, Russia, Sri Lanka, Sudan, Tajikistan, Tunisia, Turkmenistan and Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.