Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Mahakama kuu nchini Pakistan yaagiza waziri mkuu Raja Pervez Ashraf kufika mahakamani

Mahakama kuu nchini Pakistan imemuandikia barua ya kufika mahakamani hapo waziri mkuu Raja Pervez Ashraf kueleza ni kwanini ameshindwa kufungua kesi ya rushwa dhidi ya rais. 

Waziri mkuu wa Pakistan, Raja Pervez Ashraf
Waziri mkuu wa Pakistan, Raja Pervez Ashraf Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya mahakama kuu inakuja ikiwa imepita miezi miwili toka kuondolewa madarakani kwa waziri mkuu Yousuf Raza Gilan ambaye alivuliwa wadhifa wake na mahakama baada ya kukataa kufungua kesi ya rushwa dhidi ya rais Asif Ali Zardar.

Mahakama kuu ilitoa siku kumi kwa waziri mkuu mteule Ashraf kuaiza mamlaka nchini Uswis kufungua kesi dhidi ya rais Zardar na maofisa wengine wa Serikali ya nchi hiyo ambao wanatuhumiwa kushiriki vitendo vya rushwa.

Serikali imekataa kufungua mashataka ya rushwa dhidi ya rais kwa madai kuwa analindwa na katiba ya nchi hiyo lakini pia na muda wa kufungua upya kesi hiyo umeshapita kwa mujibu wa katiba.

Waziri mkuu Ashraf amesisitiza serikali yake kutofungua kesi hiyo dhidi ya rais Zardar na kwamba atakuwa tayari kuilinda katiba ya nchi hiyo sio kwa shinikizo toka kwenye mahakama kuu ya nchi.

Kesi ya rushwa dhidi ya Zardari ilifunguliwa mwaka 1990 wakati mke wake Benazir Bhutto akiwa waziri mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.