Pata taarifa kuu
UHISPANIA-ITALIA

Uhispania na Italia zakataa mpango wa kupewa msaada wa fedha toka IMF

Nchi ya Uhispania na Italia zimekataa mpango wa kupatiwa msaada wa fedha toka shirika la fedha duniani IMF na badala yake zimekubaliana na mapendekezo ya kupatiwa mkopo toka benki kuu ya Ulaya.

viongozi wa Uhispania  Mariano Rajoy na Italia Mario Monti
viongozi wa Uhispania Mariano Rajoy na Italia Mario Monti
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy na mwenzake wa Italia Mario Monti wametangaza kukubaliana na mapendekezo ya benki kuu ya Ulaya ya kutaka kuimarisha masoko kwenye jumuiya hiyo kwa lengo la kuleta usawa wa kibiashara utakaosaidia baadhi ya mataifa kupunguza madeni yake ya ndani.

Hapo jana rais wa Benki kuu ya Ulaya Mario Draghi alitangaza mpango mpya wa benki yake wa kutaka kuimarisha soko la pamoja ambalo litakuwa huria zaidi kwa lengo la kuyasaidia mataifa mengine kukabiliana na hali mbaya ya uchumi.

Wakati hayo yakiarifiwa, Polisi nchini Uhispania wamefanikiwa kuwakamata watu watatu ambao wanatuhumiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la kigaidi duniani la Al-Qaeda kusini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Cadiz na Ciudad Real.

Waziri wa mambo ya ndani wa Hispania, Jorge Fernandez Diaz amethibitsha kukamatwa kwa watu hao na kuongeza kuwa upo ushahidi wa kutosha wa kuwahusisha watuhumiwa hao na njama za kutaka kutekeleza shambulio la kigaidi nchini humo au kwenye nchi za Ulaya.

Maofisa usalama nchini humo wamekuwa wakifanya operesheni za mara kwa mara kuwasaka wafausi wa kundi hilo ambao walitekeleza shambulio baya la kigaidi kwenye mji wa Madrid mwaka 2004.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.