Pata taarifa kuu
Marekani-Afrika

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aanza ziara yake barani Afrika

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton amewasili jana jijini Dakar nchini Senegal katika ziara yake ndefu anayo ifanya barani Afrika. Clinton atapokelewa kwa mazungumzo na rais wa Senegal Macky Sall mchana na baadae atahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Cheikh Anta Diop jijini Dakar katika hutuba iliobatizwa"The Speech Of Dakar".

Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ya siku mbili nchini Senegal, Clinton anataraji kupongeza juhudi za kidemokrasia ambazo zimepigwa na Senegal katika kipindi hiki. Senegal imekuwa mfano wa demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika na mshirika wa karibu wa serikali ya Washington katika ukanda wa nchi zinazo zungumza lugha ya Kifaransa.

Hillary Clinton ameshawahi kutembelea nchini Senegal mwaka 2008, lakini kama mke wa rais, kwa sasa anazuru nchi hiyo akiwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambapo anatakiw akuwa na kauli za kidiplomasia ili kuepusha mkanganyiko kama ulioshuhudiwa mwaka 2007 wakati rais wa zamaniw a Ufaransa Nicolas Sarkozy alipozuru nchi hiyo.

Mbali na Senegal, Waziri Clinton atazuru nchi za Sudani, Sudani Kusini, Uganda, Kenya, Malawi, Afrika Kusini na hatuwa ya mwisho ya ziara hiyo itakuwa nchini Ghana ambako atashiriki katika shughuli za mazishi ya rais wa Ghana John Evans Atta Mills aliefariki mwanzoni mwa juma lililopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.