Pata taarifa kuu
Ufaransa-Italia

Rais wa Ufaransa Francois Hollande kuhakikisha uchumi wa ulaya unaimarika

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amejiapiza kufanya kila linalowezekana kulinda na kuimarisha uchumi wa Ukanda wa Ulaya baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti jijini Paris nchini Ufaransa.

rais wa Ufaransa Francois Hollande na Mario Monti
rais wa Ufaransa Francois Hollande na Mario Monti
Matangazo ya kibiashara

Hollande amesema kama walivyoafikiana kwenye Baraza la Ulaya mwezi Juni kuhakikisha wanaimarisha uchumi wa eneo hilo na hivyo nchi ya Ufaransa itakuwa mstari wa mbele kutekeleza hilo kwa vitendo.

Rais Hollande ameongeza kuwa ni wajibu wao kutetea uchumi wa Ulaya kwa nguvu zao zote kwani kutetereka kwake kutakuwa na madhara kwa mataifa mengine yaliyopo katika eneo hilo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti amekiri huu ni wakati kwa Viongozi wote wa Ulaya kukubaliana kufanyakazi kwa pamoja na kuhakikisha nchi zinazotumia sarafu ya Ulaya zinapiga hatua za kimaendeleo.

Monti amesema iwapo Viongozi hao watashindwa kuafikiana kwenye hilo ni wazi hali ya baadaye ya mataifa huko Ulaya itakuwa mbaya zaidi na hata kuwa chanzo cha uchumi wa eneo lote kuingia matatani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.