Pata taarifa kuu

Serikali ya Liberia lapokea hatua ya UN kuiondolea vikwazo

Serikali ya Liberia imepokea kwa mikono miwili hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kuondoa vikwazo kwa maofisa 17 waliokuwa wanahudumu chini ya utawala wa Rais wa zamani Charles Taylor.

REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje Augustine Naguafan ndiye ambaye ameongea kwa niaba ya serikali ya Liberia na kusema ni hatua nzuri kuona maofisa hao wa zamani wa serikali wanaondolewa vikwazo hivyo.

Baraza la Usalama liliwawekea vikwazo vya kusafiri na hata kuchukua mali zao maofisa hamsini na tano wengi wao wakiwa ni maofisa wa serikali pamoja na makamanda wa Jeshi ambao walitajwa kuchangia vita nchini Sierra Leone.

Miongoni mwa wale ambao wameondolewa vikwazo ni pamoja na watalaka wa Mbabe huyo wa Kivita Taylor, Agnes Reeves na Jewel Howard Taylor ambao walipewa talaka na sasa wapo huru kusafiri na mali zao watarudishiwa.

Vikwazo hivyo viliwekwa kwa wao hao waliokuwa wanatajwa kuwa karibu na Charles Taylor ambaye alihusika kufadhili vita vywa wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone na sasa anatumikia kivuto baada ya kukutwa na hatia na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.