Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Uingereza yaimarisha ulinzi wakati wa michezo ya Olimpiki

Uingereza inasema zaidi ya wanjeshi elfu moja watatumiwa kusaidia kulinda usalama wakati wa mashindano ya Olimpiki inyaoanza siku ya Ijumaa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa michezo Jeremy Hunt amesema tayari wanajeshi hao wameshaanza kuwasili katika viwanja mbalimbali kulinda usalama kwa kile waziri huyo anasema hawawezi kuupuza chocghote kwa sasa.

Mapema mwezi huu kampuni iliyokuwa imepewa zabuni ya kuhakikisha uslama wa wachezaji viwanja na mashambiki wa michezo hiyo G4S ilisema haikuwa na maafisa wa usalama wa kutosha kutoa ulinzi huo na hivyo kuilazimisha serikali kutumia wanajeshi wake.

Tayari maelfu ya wanamichezo kutoka pembe zote duniani tayari wamewasili nchini Uongereza tayari kwa ufunguzi wa mashindano hayo siku ya Ijumaa usiku.

Tayari wageni mashuhuri 120 wamethibitisha kuwasili kwao mjini london siku ya ijumaa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Waziri Mkuu wa Japan Yoshihiko Noda akiwemo mke wa kwanza wa rais wa Marekani Michelle Obama.

Mamilioni ya mashabiki wa michezo hiyo nchini Uingereza na duniani wanatarajiwa kushuhdia ufunguzi huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.